Home Kimataifa Bunge la Canada lachagua spika wa kwanza wa asili ya Afrika

Bunge la Canada lachagua spika wa kwanza wa asili ya Afrika

0

Wabunge katika bunge la Canada wamechagua spika wa kwanza wa asili ya Afrika.

Gregory Fergus alichaguliwa spika Jumanne Oktoba 3, 2023 kwenye uchaguzi ulioandaliwa kufuatia kujiuzulu kwa spika wa awali Anthony Rota.

Rota alilazimika kujiondoa kufuatia malalamiko ya wengi baada yake kumwalika na kutoa heshima kwa mtu ambaye alikuwa mwanachama wa kikosi cha Nazi katika vita vya pili vya dunia.

Punde baada ya hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky mbele ya bunge la Canada mwezi jana, wabunge wa Canada walisimama kutoa heshima kwa Yaroslav Hunka wa umri wa miaka 98, baada Rota kumtaja.

Rota alisema Hunka ni shujaa wa vita ambaye alipigania kujitenga kwa Ukraine.

Website | + posts