Home Kimataifa Bunge kuzuia vyuo vikuu kutoa kozi za ‘diploma na certificate’

Bunge kuzuia vyuo vikuu kutoa kozi za ‘diploma na certificate’

0
kra

Vyuo vikuu vitasitisha kutoa mafunzo ya stashahada na “certficate” endapo mswada wa mbunge wa Embakasi Central Benjamin Gathiru utaidhinishwa na bunge la kitaifa.

Mswada huo wa mwaka 2023 wa marekebisho nambari 5 unapendekeza vyuo vikuu kutoa mafunzo ya stashahada za juu maarufu kama postgraduate Diplomas na vyeti vya juu ukipenda postgraduate certificate.

kra

Mapendekezo hayo yalikuwa kwenye ripoti ya jopo la Rais kuhusu elimu (PWPER) kama mojawapo ya njia za kuboresha elimu.

Mbunge huyo anasema kurekebisha sheria za vyuo vikuu za mwaka 2012 kutasaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya kiufundi nchini au TVET huku vyuo vikuu vikisalia kutoa mafunzo ya shahada za juu na shahada.

Website | + posts