Home Burudani Bull Dogg ajitolea kusaidia familia ya marehemu Jay Polly

Bull Dogg ajitolea kusaidia familia ya marehemu Jay Polly

0
kra

Msanii wa mtindo wa Hip Hop nchini Rwanda Bull Dogg, ambaye jina lake halisi ni Malik Bertrand Ndayishimiye ameahidi kuendelea kutunza watoto wa marehemu msanii mwenzake Jay Polly.

Bull Dogg alimkumbuka rafiki yake Jay Polly wanapoadhimisha miaka mitatu tangu alipofariki wakati alitoa hakikisho hilo.

kra

Dogg alimrejelea Jay Polly kama mwanafunzi wa maisha, mtu mvumilivu aliyeshauri wenzake na kuwasaidia pia hata kama yeye mwenyewe alipitia magumu tangu utotoni.

“Polly alikuwa rafiki yangu wa karibu, tulipitiamaisha pamoja, tulibadilishana ushauri na kusaidiana katika kazi yetu ya sanaa.” alisema Dogg.

Alisisitiza kwamba angependa sana kuwa karibu na familia yake na kuwa kielelezo kwa wanawe huku akiwahadithia kuhusu baba yao mzazi.

Dogg alikuwa kwenye kundi moja la muziki kwa jina Tuff Gang pamoja na Jay Polly, Fireman, P Fla na Green P.

Jay Polly ambaye jina lake halisi ni Tuyishime Joshua, aliaga dunia tarehe 2 mwezi Septemba mwaka 2021 akiwa jela nchini Rwanda kutokana na kile kilichosemenaka kuwa kubugia kinywaji chenye sumu.

Yeye na wafungwa wengine wawili wanaripotiwa kuchanganya kemikali ya Methanol na vinywaji vingine wakanywa wakiwa kizuizini, maelezo yaliyokataliwa na familia yake ambayo inahisi kwamba aliuawa.

Jay Polly alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2021 kutokana na kukosa kufuata kanuni zilizokuwa zimewekwa za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Aliandaa sherehe kinyume na kanuni hizo.

Kila mwaka watu wa familia yake na marafiki hukutana kwenye kaburi lake huko Rusororo jijini Kigali kumkumbuka na zamu hii wameashiria kwamba huenda wakaandaa tamasha la kumkumbuka.

Website | + posts