Home Michezo Brigid Kosgei atwaa ubingwa wa makala ya 33 ya Lisbon Half Marathon

Brigid Kosgei atwaa ubingwa wa makala ya 33 ya Lisbon Half Marathon

0

Aliyekuwa mshikilizi wa rekodi ya Dunia Brigid Kosgei, ameibuka mshindi wa makala ya 33 ya mbio za Lisbon Half Marathon zilizoandaliwa Jumapili nchini Ureno.

Kosgei aliyetumia shindano hilo kujiandaa kwa London marthon mwezi April,alikata utepe kwa dakika 64 na sekunde 49.

Bosena Mulatie na Tigist Mengistu wote kutoka Ethiopia walimalzia katika nafasi za pili na tatu wakisajili muda wa dakika 65 na sekunde 46 na dakika 66 na sekunde 20 mtawalia.

Dominic Chemutb Kiptarus alimaliza nafasi ya pili katika mbio za wanaume akitumia dakika 60 na sekunde 40, nyuma ya Dinkalem Ayele kutoka Ethiopia aliyetwaa ubingwa kwa dakika 60 na sekunde 36