Brendan Rodgers amerejea kuifunza klabu ya Celtic, miaka minne tangu aigure timu hiyo na kujiunga na Leicester City.
Rodgers aliye na umri wa miaka 50, ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuwanoa mabingwa hao wa ligi kuu wa Scotland kutwaa nafasi ya Ange Postecoglou aliyehamia Tottenham Hotspur mapema mwezi huu.
Rodgers alipigwa kalamu na Leicester mwezi April mwaka huu.
Katika kipindi chake cha kwanza alichohudumu Celtic kati ya mwaka 2016 na 2019, Rodgers alinyakua mataji saba mtawalia.