Home Michezo Brazil washinda, Colombia wapigwa huku Argentina wakikabwa koo

Brazil washinda, Colombia wapigwa huku Argentina wakikabwa koo

0
kra

Mabingwa wa dunia Argentina wamelazimishwa kutoka sare ya bao moja ugenini dhidi ya Venezuela katika mechi za Amerika Kusini kufuzu kwa Kombe la Dunia mapema Ijumaa.

Argentina walitangulia kufunga kunako dakika ya 13  kupitia Nicholas Otamendi kabla ya Solomn Rondon kukomboa kwa wenyeji Venezuela.

kra

Mabingwa mara tano wa Dunia Brazil walirejelea tambo za ushindi, wakiibwaga Chile 2-1, Igor Da Cruz na Luis Enrique wakifunga mabao ya Samba naye Eduardo Vargas akafunga goli la Chile.

Colombia wakicheza ugenini Bolivia waliambulia kichapo cha bao moja kwa bila wakati Paraguay na Ecuador wakitoka sare tasa.

Argentina wangali kuongoza kwa alama 19, pointi tatu zaidi ya Colombia iliyo ya pili huku Uruguay ikiwa na alama 15 katika nafasi ya tatu.

Brazil ni ya nne kwa pointi 13 ikifuatwa na Bolivia na Venezuela kwa alama 12 kila moja.

Website | + posts