Home Habari Kuu Bore: Serikali inajizatiti kukabiliana na ajira ya watoto

Bore: Serikali inajizatiti kukabiliana na ajira ya watoto

0
kra

Waziri wa Leba na ulinzi wa jamii Florence Bore, amesema serikali imejitolea kuhakikisha watoto hapa nchini wanalindwa dhidi ya ajira ya watoto.

Akizungumza leo Ijumaa wakati wa kuadhimisha siku ya Kimataifa dhidi ya ajira ya watoto kwenye uwanja wa Kericho Green, kaunti ya Kericho, waziri huyo alisema kuwa wizara yake itashirikiana na serikali za kaunti kutekeleza sera kuhusu utunzaji watoto ili kuepusha ajira kwa watoto.

kra

“Ili kupunguza ajira ya watoto, tumebuni mfumo unaojumuisha jamii kuhamasisha kuhusu uwezeshaji kupitia elimu, uchumi, teknolojia, uvumbuzi na utekelezwaji wa sheria,” alisema waziri Bore.

Waziri huyo aliwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha hakuna mtoto anafanya aina yoyote ya ajira na badala wawapeleke shuleni.

“Kuna tofauti kati ya kufunza mtoto kazi na kutumia mtoto kwa kazi. Wakati wa likizo, wape mafunzo ya kufanya kazi. Lakini usimzuie mtoto kwenda shuleni ili wafanye kazi,” alidokeza waziri huyo.

Alisema kuwa utumiaji wa watoto kwenye mashamba ya majani chai na kahawa na sehemu nyingine umekithiri, akiongeza kuwa sera za soko kuhusu mazao hayo haziruhusu kitendo hicho.

Siku ya kukabiliana na ajira kwa watoto duniani iliadhimishwa leo katika kaunti ya Kericho, ambapo maudhui yalikuwa ‘Kenya inaazimia kukomesha ajira kwa watoto na huu ndio wakati wa kuchukua hatua.’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here