Home Michezo Bondia Nick Okoth hatimaye alipwa na BFK

Bondia Nick Okoth hatimaye alipwa na BFK

0

Bondia Nick Okoth hatimaye amepokea malipo yake ya tarkriban shilingi laki sita kutoka kwa shirikisho la ngumi nchini Kenya,BFK.

Okoth ambaye alistaafu mchezo wa ngumi mwaka uliopita, amekuwa akisubiri malipo yake ya kunyakua nishani ya shaba katika mashindano ya bara Afrika ya mwaka 2022 mjini Maputo Msumbiji, alikoshinda medali ya fedha.

Maafisa wa BFK walimkabidhi Okoth pesa taslimu siku ya Jumatano, baada yake kuzua lalama katika mitandao ya kijamii kwa kucheleweshwa kulipwa.

Website | + posts