Home Habari Kuu Bodi ya dawa na sumu yatoa tahadhari kuhusu dawa ghushi ya kutibu...

Bodi ya dawa na sumu yatoa tahadhari kuhusu dawa ghushi ya kutibu Saratani

Wananchi wametahadharishwa dhidi ya kutumia, kusambaza au kuuza dawa hiyo kwani siyo salama. 

0

Wananchi wametahadharishwa dhidi ya dawa ghushi ya kutibu saratani ya matiti, inayosambazwa katika soko la hapa nchini.

Bodi ya dawa na sumu hapa nchini (PPB), katika taarifa leo Jumamosi, ilisema kampuni ya Ujerumani ya German Roche Products inayotengeneza dawa hiyo, imethibitisha kuwa dawa za Herceptin zilizoko sokoni ni ghushi.

Kulingana na bodi hiyo, tarehe ya kutenegenezwa kwa dawa hiyo ni mwezi Disemba mwaka 2021, huku tarehe ya kukamilika kwa matumizi ikiwa mwezi Novemba mwaka huu.

Wananchi wametahadharishwa dhidi ya kutumia, kusambaza au kuuza dawa hiyo kwani siyo salama.

“Bodi hii inawatahadharisha wakenya dhidi ya kutumia, kusambaza au kuuza dawa hizo, kwa kuwa usalama na ubora wake hauwezi bainishwa,” ilisema bodi hiyo kwa taarifa.

Kadhalika, bodi hiyo ilisema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaopatikana na kosa la kukiuka kanuni zilizowekwa na bodi hiyo.

Wakati uo huo wananchi na wahudumu wa afya wamehimizwa kuripoti na visa vyovyote vya usambazaji  bidhaa ghushi za matibabu.