Home Burudani Bobi Wine apigwa risasi mguuni

Bobi Wine apigwa risasi mguuni

0
kra

Mwanamuziki Bobi Wine ambaye pia ni mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda anaripotiwa kupigwa risasi kwenye mguu na maafisa wa polisi katika eneo la Bulindo, Kira wilaya ya Wakiso.

Video ilichapishwa mitandaoni ikimwonyesha Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi akinyanyuliwa na wasaidizi wake na kuingizwa kwenye gari ambayo inaaminika kumpeleka hospitalini.

kra

Taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya kiongozi huyo wa chama cha National Unity Party NUP inathibitisha kisa hicho ikimalizikia kwenye ahadi ya kutoa taarifa zaidi.

Video nyingine inamwonyesha akiwa amefikishwa hospitalini ambapo alikuwa amevuliwa viatu lakini hakuwa anaweza kutembea na hivyo kusaidiwa na wasaidizi wake.

Website | + posts