Kiungo wa zamani wa Ghana Kevin-Prince Boateng, amestaafu kutoka soka akiwa na umri wa miaka 36.
Boateng mzawa wa Berlin alitangaza kustaafu kwake kupitia kwa mtandao wake wa Instagram siku ya Ijumaa na timu yake ya mwisho aliyoichezea ikiwa Hertha Berlin alikoanzia amali yake ya soka.
Boateng alichezea klabu 15 zikiwemo AC Milan,Barcelona kando na kucheza Uingereza ,Uturuki,Italia na Ujerumani.
Kwa upande wa timu ya taifa Boateng aliichezea Black Stars mechi 15 akipachika mabao mawili kati ya mwaka 2010 na 2014.