Home Habari Kuu Bitok: Uchapishaji wa vitambulisho vipya kuharakishwa

Bitok: Uchapishaji wa vitambulisho vipya kuharakishwa

Takriban maombi 8,000 ya vitambulisho hupokewa kila siku.

0
Serikali kuharakisha uchapishaji wa vitambulisho vipya.
kra

Serikali imesema itakamilisha shughuli ya uchapishaji wa vitambulisho vipya vya kitaifa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Katibu wa Idara ya Uhamiaji na Huduma kwa Wananchi Julius Bitok, amesema ucheleweshwaji wa shughuli hiyo umetokana na hitilafu za mashine ya kuchapisha stakabadhi hizo ambayo sasa imefanyiwa ukarabati, pamoja na kesi iliyowasilishwa mahakamani ya kusimamisha shughuli hiyo.

kra

Kwa sasa, nakala 15,000 za vitambulisho hivyo al maarufu Maisha Card zinachapishwa kila siku huku nakala laki sita zikiwa tayari zimechapishwa.

“Nawahakikishia Wakenya kwamba mashini zetu sasa zinafanya kazi, na tutapata vitambulisho bila kuchelewa jinsi ilivyokuwa hapo awali,” alisema Bitok.

Katibu huyo aliwahakikishia Wakenya kwamba shughuli ya uchapishaji wa kadi hizo inaendelea saa 24 ili kumaliza mrundiko ulioko.

kulingana naye, takriban maombi 8,000 ya vitambulisho hupokelewa kila siku.

Serikali pia inatarajia kununua mashine nyingine mpya ya uchapishaji mwezi ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here