Home Kimataifa Binamuye Sagini ahukumiwa kifungo cha miaka 40

Binamuye Sagini ahukumiwa kifungo cha miaka 40

0

Binamu wa mtoto Sagini kwa jina Alex Ochogo amehukumiwa kifungo cha miaka 40 gerezani kwa kosa la kumng’oa macho mtoto huyo.

Shangazi ya Sagini aitwaye Pacificah Nyakerario na nyanyake Rael Nyakerario walihukumiwa vifungo vya miaka 10 na 5 mtawalia kwenye hukumu iliyotolewa jana na Hakimu Mkuu Mkazi wa Kisii, Christine Ogweno.

Hakimu huyo alijuta kwamba hatima ya mtoto huyo imebadilika kabisa kwani hawezi tena kuona na kwa sababu hiyo akaomba mashirika ya usaidizi yasimtelekeze mtoto huyo wa umri wa miaka mitatu.

Sagini alikuwa ameachwa na mamake mzazi chini ya malezi ya babake wa kambo ambaye ni mgonjwa na kwa sababu hiyo akawa anapokea malezi kutoka kwa nyanyake mzaa baba wa kambo.

Alitoweka jioni moja wakati alikuwa anacheza na watoto wengine katika kijiji cha Ikuruma, kaunti ya Nyamira na baadaye akapatikana kwenye shamba moja la mahindi akiwa bila macho na akivuja damu.

Mtoto huyo alitoa ushahidi mahakamani ambapo alisema nyanyake ndiye alimng’oa macho.

Mashtaka ya watatu hao, yalibadilishwa kortini mwezi Februari mwaka huu kutoka kujaribu kuua na kuwa kumsababishia mtoto huyo madhara makubwa mwilini kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Korti iliwapata na hatia mnamo Julai 7, 2023.

Website | + posts