Home Habari Kuu Bima ya afya ya jamii, SHIF kutekelezwa mwezi Julai

Bima ya afya ya jamii, SHIF kutekelezwa mwezi Julai

Hatua hiyo ni baada ya kuanzishwa kwa zoezi la kuwasajili wakenya katika hazina hiyo kuanzia mwezi Machi.

0

Serikali imesema hazina ya bima ya afya ya jamii, SHIF itaanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka huu.

Kulingana na serikali, usajili wa Wakenya katika bima hiyo utaanzishwa mwezi Machi mwaka huu.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amedokeza kuwa wadau wote wamehusishwa, na kwamba arifa itakayotumwa kwa mwanasheria mkuu ili kuchapishwa kwa gazeti rasmi la serikali, itakuwa jumuishi.

Hata hivyo, Baraza la Magavana limelalamikia kuharakishwa kutekelezwa kwa bima hiyo, likisema Wizara ya Afya haijawahusisha katika mchakato huo.

Kupitia kwa mwenyekiti wao wa kamati ya afya Muthomi Njuki, Magavana hao walitaka swala la malipo kwa hospitali za umma kushughulikiwa haraka iwezekanavyo, wakidokeza kuwa hospitali za kibinafsi huenda zikanufaika pakubwa jinsi ilivyoshubudiwa katika bima ya afya ya NHIF.

Aidha, serikali imedokeza kuwa itashirikiana na serikali za kaunti kutekeleza bima ya SHIF.

Website | + posts