Home Michezo Bett na Chepng’eno washinda mbio za nyika Ol -kalou

Bett na Chepng’eno washinda mbio za nyika Ol -kalou

0

Edwin Bett na Cynthia Chepng’eno wametwaa ubingwa wa kilomita 10 katika mkondo wa nne wa mbio za nyika ulioandaliwa Jumamosi mjini Ol-Kalou kaunti ya Nyandarua .

Bett ameshinda kwa kutumia dakika 29 sekunde 39 nukta 58 ,akifuatwa na Cornelius Kemboi kwa dakika 29 sekunde 43 nukta 94, huku Emmanuel Kiprop akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 29 sekunde 46 nukta 86 .

Chepngeno amenyakua ushindi katika kilomita 10 kwa wanawake akitumia dakika 33 sekunde 28 nukta 78,akifuatwa na Loice Chemnung, aliyetumia dakika 33 sekunde 28 nukta 85 wakati Sela Jepleting akimaliza wa tatu kwa dakika 33 na sekunde 46.

Nancy Cherop aliibuka mshindi wa kitengo cha kilomita 6 wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 kwa dakika 20 sekunde 7 nukta 77 ,akifuatwa na Yvonne Chepchirchir na Joyline Chepkemoi katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

Mbio za wavulana walio chini ya umri wa miaka 20 kilomita nane zimeshindwa na Mathew Kipkoech, aliyetumia dakika 23 sekunde 57 nukta 84, akifuatwa na Vincent Kibet na Kelvin Kiprop katika nafasi za pili na tatu katika usanjari huo

Website | + posts