Home Biashara Benki ya Equity yang’aa kwa kujizolea tuzo tatu India

Benki ya Equity yang’aa kwa kujizolea tuzo tatu India

0
???????????????

Benki ya Equity iko na kila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea tuzo tatu za kifahari kwenye Tuzo za Ufadhili wa Biashara Ndogo na za Kati Duniani 2023, yaani Global SME Finance Awards 2023.

Tuzo hizo huandaliwa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC), ambalo ni mwanachama wa Kundi la Benki ya Dunia na Kongamano la Ufadhili wa Biashara Ndogo na Kati, yaani SME Finance Forum.

Lengo ni kutambua mafanikio ya kupigiwa mfano katika kupanua upatikanaji wa fedha kwa biashara ndogo na za kati.

Benki ya Equity ilipokea tuzo mbili za Platinum katika makundi ya Mfadhili wa Biashara Ndogo na Kati wa Mwaka barani Afrika na Uvumbuzi wa Bidhaa wa Mwaka kutokana na mpango wake wa “Lipa na Equity”.

Kisha ilipata tuzo katika kundi la Mfadhili wa Wanawake wa Mwaka.

Washindi wa Tuzo za Ufadhili wa Biashara Ndogo na za Kati Duniani 2023 walitangazwa wakati wa Kongamano la Ufadhili wa Biashara Ndogo na Kati Duniani 2023 lililoandaliwa mjini Mumbai, India.

Website | + posts