Home Michezo Benjamin Mendy aondolewa mashtaka ya ubakaji

Benjamin Mendy aondolewa mashtaka ya ubakaji

Jopo la Mahakama la majaji 12 lilijadili kwa takriban saa tatu na dakika 15 kabla ya kufikia uamuzi huo.

0
Benjamin Mendy. Picha/Hisani.

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester City Benjamin Mendy, ameondolewa mashtaka ya kumbaka mwanamke na kujaribu kumbaka mwingine.

mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alishtakiwa kwa kumshambulia mwanamke mwenye umri wa miaka 24 katika jumba lake la kifahari lililoko Mottram St Andrew, Cheshire mwezi Oktoba mwaka 2020.

Mendy pia alishtakiwa kwa jaribio la kumbaka mwanamke mwingine, mwenye umri wa miaka 29, ambaye pia alisema kuwa alimdhalilisha nyumbani kwake miaka miwili kabla.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliangua kilio wakati hukumu ya kutokuwa na hatia ikisomwa na msimamizi wa mahakama kufuatia kesi iliyodumu kwa wiki tatu katika Mahakama ya Chester Crown.

Jopo la Mahakama la majaji 12 lilijadili kwa takriban saa tatu na dakika 15 kabla ya kufikia uamuzi huo.

Jaji Steven Everett alisema: “Bw Mendy anaweza kuachiliwa kutoka kizimbani.”

Mwanasoka huyo, ambaye mkataba wake na Manchester City ulimalizika mapema mwezi huu, aliondolewa katika kesi ya awali ya makosa sita ya ubakaji na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono, unahuhusisha na wasichana wanne.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here