Home Biashara Bei za Petroli na mafuta taa zapunguzwa

Bei za Petroli na mafuta taa zapunguzwa

0

Bei za petroli ya supa na mafuta taa zimepunguzwa kwa senti 85 na shillingi 3.96 mtawalio.

Halmashauri ya kuthibiti bei za petroli EPRA inasema lita moja ya petroli ya Supa sasa inauzwa kwa shillingi 194.68 ilhali lita moja ya mafuta taa inauzwa kwa shillingi 169.48.

Bei ya Diesel itasalia kuwa shillingi 179.67 kwa lita.

Mabadiliko hayo ya bei za mafuta yamefanywa siku 14 baada ya bei hizo kuongezwa kwa shillingi 13 kwa lita tarehe 29 mwezi Juni kufuatia kuongezwa kwa ushuru ziada wa thamani wa bidhaa za mafuta hadi asilimia 16 kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2023.

Halmashauri ya EPRA iliongeza bei za mafuta licha ya uamuzi wa mahakama kuu wa kusimamisha utekelezaji wa sheria hiyo.

Website | + posts