Home Michezo Beatrice Chebet ashinda mbio za nyika nchini Uhispania

Beatrice Chebet ashinda mbio za nyika nchini Uhispania

0

Jumapili Oktoba 29, 2023, bingwa wa mbio za nyika duniani Beatrice Chebet aliibuka mshindi wa mbio za nyikani za Uhispania almaarufu “Cross Internacional de Atapuerca” upande wa kina dada.

Aliweza kupata ushindi huo, hata ingawa mbio hizo ziliandaliwa katika mazingira magumu ambapo upepo mkali ulikuwa ukivuma kwa kasi ya kilomita 45 kwa saa pamoja na mvua.

Mshindi huyo wa nishani ya shaba katika mbio za mita 5000 duniani Chebet alihifadhi taji yake.

Aliongoza kuanzia mwanzo katika mashindano ya wanawake huku wakenya wenzake Edinah Jebitok na Lucy Mawia wakimfuata kwa karibu.

Chebet ambaye alitanua pengo kubwa katika uongozi wa mbio hizo kwenye mzunguko wa mwisho na kufika utepeni sekunde 15 mbele ya Chelangat huku Jebitok akikamilisha orodha ya watatu wa mwanzo na alifika utepeni sekunde nane nyuma ya Chelangat.

Chebet aliridhika na ushindi huo na ule wa awali na akasema sasa anaangazia mbio za nyikani za Seville Novemba 12, 2023.

Katika upande wa wanaume, Jacon Kiplimo wa Uganda ndiye aliibuka mshindi wa mbio hizo nchini Uhispania.

Website | + posts