Home Michezo Bayern Munich wamo mbioni kumtafuta kocha

Bayern Munich wamo mbioni kumtafuta kocha

Hali hii imetokana na kushindwa mara tatu kwa mpigo dhidi ya Leverkusen(3-0), Lazio(1-0) na VfL Bochum(3-2).

0
Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel.

Miamba wa soka nchini Ujerumani Bayern Munich, wamo mbioni kumteua kocha mwingine atayechukua nafasi ya kocha wa sasa Thomas Tuchel.

Hali hii imetokana na kushindwa mara tatu kwa mpigo dhidi ya Leverkusen(3-0), Lazio(1-0) na VfL Bochum(3-2).

Kwenye ligi ya Ujerumani, Bayern inashikilia nafasi ya pili kwa alama 50 nyuma ya Levérkusen ya kocha Xabi Alonso iliyo na alama 58.

Huenda hii ikawa mara ya kwanza timu hiyo kutoshinda tuzo lolote kwa kipindi cha miaka 12, jambo ambalo limewakosesha usingizi wakuu na mashabiki wake.

Sasa hivi mipango ya kumteua kocha mwengine imepamba moto.

Wale ambao wanaomezewa mate ni pamoja na aliyekuwa kocha Manchester United na mwangalizi wa kiufundi wa sasa UEFA Ole Gunnar Solskjaer, mkufunzi wa zamani wa Real Madrid na mshindi mara tatu wa klabu bingwa ulaya na klabu hiyo Zinedine Zidane na Xabi Alonso wa Bayer liverkusen ambao hawajashindwa mechi 32 na Pia wanaongoza Bundesliga.

Boniface Musotsi
+ posts