Home Michezo Bayer Leverkusen watwaa ubingwa wa ligi kuu Ujerumani kwa mara ya kwanza

Bayer Leverkusen watwaa ubingwa wa ligi kuu Ujerumani kwa mara ya kwanza

0

Klabu ya Bayer Leverkusen ilitawazwa mabingwa wa ligi kuu Ujerumani kwa msimu wa mwaka 2023/2024 kwa mara ya kwanza Jumapili jioni kufuatia ushindi wa mabao matano kwa bila dhidi ya Werder Bremen.

Ushindi huo uliwaweka Leverkusen kwa uongozi wa Bundesliga kwa pointi 79,alama 16 mbele ya mabingwa wa mwaka jana Bayern Munich baada ya mechi 29 ,zikisalia mechi 3 msimu ufikie tamati.

Leverkusen wanaofunzwa na Xabi Alonso pia wananusia kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la Europa League wakiongoza mabao 2 kwa bila dhidi ya Westham United katika duru ya kwanza.