Home Habari Kuu Bawabu Eric Mulyanga alipwa fidia ya shilingi 130,000 kwa kufurushwa kazini

Bawabu Eric Mulyanga alipwa fidia ya shilingi 130,000 kwa kufurushwa kazini

0

Mahakama ya Milimani imeamrisha bawabu Benjamin Eric Mulyanga aliyefanya kazi na kampuni ya Zitron Limited, alipwe fidia ya shilingi 130,000 kwa kutimuliwa kazini kwa njia isiyostahili.

Mulyanga, aliyefanya kazi kwa kipindi cha miaka sita na kampuni ya Zitron aliachishwa kazi Februari 27, 2018.

Wakati wa kutimuliwa, Mulyanga alikuwa amepandishwa cheo kuwa msimamizi wa kampuni hiyo.

Kufuatia kutimuliwa kwake, alilazimika kuhamia mashinani baada ya mwanawe kutimuliwa shuleni kwa kukosa karo na pia kumpoteza mkewe kutokana na mshtuko wa moyo.

Mfanyakazi huyo wa zamani alitaka alipwe shilingi 560,000, zikiwemo mshahara wa miezi mitatu wa shilingi 90,000, shilingi 16,000 kama marupurupu ya likizo, shilingi 4,000 malipo ya likizo ya uzazi, shilingi 90,00 malipo ya kusimamizwa kazi, na fidia ya mshahara wa mwaka mmoja ya shilingi 360,000.

Hata hivyo, Jaji Jacob Gakeri aliagiza kampuni ya Zitron imlipe Mulyanga shilingi 30,000 zikiwa ni ilani ya malipo ya mwezi mmoja, shilingi 16,000 za likizo na mshahara wa miezi mitatu wenye kima cha shilingi 90,000 ambazo jumla yake ni 136,000.

 

Website | + posts