Baraza la walemavu nchini NCPWD liliandaa mkutano wa uhamasisho kuhusu mpango mpya wa mtaji wa kuanza biashara kando na vifaa vya kazi huko Mchakos kwa lengo la kuwasaidia kujiajiri.
Mpango huo mpya wa kuwapa walemavu mtaji ulianzishwa mwezi juni mwaka huu na walemavu wanahimizwa kujisajili ili wanifaike.
Akizungumza kwenye mkutano huo katika shule ya walemavu ya Masaku Emma Bosere, mmoja wa maafisa katika baraza la walemavu alisema kwamba wanahamasisha wakazi wa Machakos wakiwafahamisha kuhusu mtaji unaotolewa na vifaa vya kazi.
Vifaa vuinavyotolewa vi vya sekta kama mapishi, urembo, ufundi wa mbao, utengenezaji wa viatu, kilimo na ufundi wa magari.
Kiwango anachopatiwa mtu kulingana na Bosere kinalingana na aina ya biaishara anayotaka kuanzisha. Pesa hizo zinatosha kulipa kodi ya miezi mitatu ya nyumba ya biashara kabla ya kuimarika na kuanza kutengeneza faida.
Ili kunufaika ni lazima mtu ajisajili na awe na kadi ya kitaifa ya utambulisho kama mlemavu na biashara ambayo tayari ameanzisha. Fomu za maombi ya mtaji na vifaa zitapitia kwa mkurugenzi wa huduma za walemavu wa kaunti ambaye ataziwasilisha kwa makao makuu.
Bosere hata hivyo alilalamikia changamoto zinazkumba walemavu wanapokosa stakabadhi muhimu, akaunti ya benki ya kuwekewa pesa hizo na kukosa cheti cha usajili wa biashara.
Mmoja wa waliohudhuria mkutano huo wa uhamasisho kwa jina Abdala Mohamed, alisema anatizamia kunufaika na mpango huo akitarajia kwamba utabadilisha maisha yake.