Home Habari Kuu Baraza la Mawaziri: Usambazaji mbolea ya bei nafuu waongezeka maradufu

Baraza la Mawaziri: Usambazaji mbolea ya bei nafuu waongezeka maradufu

0

Baraza la Mawaziri Leo Jumanne limearifiwa kuwa mbolea ya bei nafuu, imesambazwa katika kaunti 42, huku usambazaji huo  ukiongezeka kwa asilimia 100.

Hadi sasa, magunia milioni 2.9 yamesambazwa kwa wakulima 538,061 ikilinganishwa na magunia milioni 1.09 kwa wakulima 270,000 mwezi Aprili mwaka jana.

Wakulima waliosajiliwa kwenye tovuti ya mtandaoni ya mbolea wamefikia milioni 5.9 ikilinganishwa na milioni 2.3 mwaka jana.  Aidha, vocha za kielektroniki milioni 9.5.

Kuhusu wasambazaji wa mbolea ya chini ya kiwango, Rais Ruto aliagiza kwamba hatua kali zichukuliwe dhidi ya “yeyote anayeharibu programu muhimu ya kitaifa”.

Aidha, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha yafuatayo:

  • Kuridhia kwa Kenya kwa Mkataba wa Kuanzisha IGAD
  • Kuridhia kwa Kenya Mkataba wa WTO kuhusu Ruzuku ya Uvuvi
  • Kuandaa Kongamano la Kikanda Ndogo cha Afrika Mashariki kuhusu Teknolojia ya Akili Bandia
  • Utoaji wa Ofisi ya Muungano wa Utafiti wa Kiuchumi wa Afrika
  • Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi ya 59
  • Maendeleo ya Utekelezaji wa Mpango wa Kupanda Miti Bilioni 15
Website | + posts
PCS
+ posts