Home Habari Kuu Baraza la magavana lachukua hatua ya kujaribu kutatua mgomo wa maafisa kliniki

Baraza la magavana lachukua hatua ya kujaribu kutatua mgomo wa maafisa kliniki

0

Baraza la magavana lilitoa mwaliko kwa maafisa wa chama cha maafisa kliniki nchini KUCO kwa mazungumzo ya kujaribu kutatua masuala yaliyosababisha mgomo ulioanza leo.

Kupitia barua iliyochapishwa na chama cha KUCO kwenye mtandao wa X, baraza la magavana limealika maafisa hao kwa mkutano leo alasiri katika afisi za baraza hilo.

Barua hiyo imetiwa saini na afisa mkuu mtendaji wa baraza la magavana nchini Mary Mwiti.

Maafisa kliniki walitangaza kuanza kwa mgomo wao leo ambapo wanachama wake wote walitakiwa kutofika kazini hadi matakwa yao yatekelezwe na serikali.

Maafisa wa KUCO walikutana na magavana Jumanne Mei 14, 2024 ambapo waliwasilisha matakwa yao na mkutano wa leo ni wa kuwasilisha maamuzi yao kwa COG kuhusu mpango uliopendekezwa wa kurejea kazini.

Website | + posts