Home Habari Kuu Barabara kuu jijini Nairobi kufungwa kuanzia Jumamosi usiku

Barabara kuu jijini Nairobi kufungwa kuanzia Jumamosi usiku

0
kra

Barabara nyingi za kuingia na kutoka katikati ya jiji la Nairobi zitafungwa kati ya Jumamosi saa nne usiku hadi Jumapili saa tisa alasiri, kupisha makala ya tatu ya mbio za Nairobi City Marathon.

Barabara zitakazofungwa kuanzia saa nne usiku wa Jumamosi ni zile za Express Way kutoka uwanja wa ndege wa JKIA hadi James Gichuru na mzunguko wa Bunyala.

kra

Barabara nyingine za kuingia na kutoka katikati ya jiji zitafungwa kuanzia saa sita usiku wa manane hadi saa nane  adhuhuri Jumapili.

Maeneo ya barabara zitakazofungwa ni mzunguko wa National Museum, Harry Thuku Road, University Way, Koinange street, Wabera Street, City Hall Way, Taifa Road, Harambee Avenue, Tumbo Avenue, Kenyatta Avenue, Uhuru Highway, Haile Selassie na Douglas Wakihuri.

Barabara nyingine zitakazofungwa ni Lang’ata road, Popo Road, Bellevue, Likoni Road na General Motors.

Makala ya tatu ya mbio za Nairobi City Marathon yataandaliwa Jumapili hii huku yakiwahusisha washiriki 15,000 waliojisajili katika vitengo vya kilomita 42,21,10 na 6.

Website | + posts