Home Habari Kuu Bangi ya thamani ya milioni 5 yanaswa Nyamira

Bangi ya thamani ya milioni 5 yanaswa Nyamira

0

Polisi katika kaunti ndogo ya Borabu, kaunti ya Nyamira wamenasa bangi ya thamani ya shilingi milioni 5.

Gari aina ya Nissan Tiida lenye nambari ya usajili KBY 435M lilikamatwa na polisi kutoka kituo cha matutu kwenye barabara ya kutoka Keroka kuelekea Sotik liliposimamishwa kwenye kizuizi.

Washukiwa wawili, mwanamume na mwanamke, ambao walitambuliwa kama Samwel Omondi Audi na Judith Kerubo walikamatwa baada ya bangi hiyo kupatikana garini.

Bangi hiyo ilikuwa imepakiwa katika magunia matano na washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Haya yanajiri wakati vita dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya vimechacha nchini, ikizingatiwa kuwa watu kadhaa wameripotiwa kuaga dunia kutokana na unywaji wa pombe haramu.