Home Kimataifa Balozi wa Ufaransa UN atoa wito wa kusitishwa mapigano

Balozi wa Ufaransa UN atoa wito wa kusitishwa mapigano

0
Moto wa jeshi la Israel unamulika angani magharibi mwa Gaza kaskazini mwa Ukanda wa Gaza

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, UN ametoa wito wa kuwepo kwa “maafikiano ya kibinadamu” huko Gaza.

Kufuatia kikao cha Baraza la Usalama kilichokuwa cha faragha, Balozi Nicolas De Rivière alisema mapatano hayo yanapaswa kudumu na kupelekea kusitishwa kwa mapigano.

Msimamo huu unaonekana kutofautiana na washirika wengine wa Magharibi kama vile Marekani na Uingereza, ambao wanasema usitishaji wa mapigano ungefaidi Hamas pekee.

Mapema Jumatatu, John Kirby, msemaji wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani, alisema Marekani haiamini kwamba usitishaji vita wa jumla ulikuwa “unafaa kwa wakati huu”.

De Rivière pia alisema kuwa Ufaransa itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kibinadamu huko Paris siku ya Alhamisi katika juhudi za kupata msaada wa ziada kwa Gaza.

BBC
+ posts