Home Kaunti Balala na wengine waondolewa mashtaka ya ufisadi na mahakama ya Malindi

Balala na wengine waondolewa mashtaka ya ufisadi na mahakama ya Malindi

0
kra

Aliyekuwa waziri wa utalii Najib Balala na watu wengine 16 ambao walikuwa wameshtakiwa kwa madai ya ufisadi wameondolewa mashtaka hayo na mahakama ya Malindi.

Hatua hii inafuatia uamuzi wa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP wa kuomba washtakiwa waondolewe makosa.

kra

Katika barua iliyoandikwa leo Julai 31 2024, ODPP ilielekeza kutoendelezwa kwa kesi hiyo kwani uchunguzi haujakamilika na ufichuzi kamili kufanyika.

ODPP inaelezea kwamba muda utakaochukuliwa kukamilisha uchunguzi haujulikani na katika uamuzi wake, hakimu James Mwaniki alikubali ombi hilo la kuondoa kesi mahakamani.

Hakimu alielekeza washtakiwa waondolewe mashtaka kulingana na sehemu ya 87(a) ya sheria ya jinai.

Alielekeza pia kwamba pesa ambazo washtakiwa walitoa kama dhamana warejeshewe pamoja na stakabadhi zozote walizotoa mahakamani.

Alifafanua kwamba kuondolewa kwa kesi hiyo kufuatia ombi la ODPP sio matumizi mabaya ya mahakama lakini iwapo ODPP itaanzisha kesi dhidi ya washtakiwa tena kwa kutumia ushahidi wa awali hatua hiyo inaweza kuchukuliwa kuwa matumizi mabaya ya mahakama.

Website | + posts
Dickson Wekesa
+ posts