Home Kimataifa Balala, watuhumiwa wengine wawili waachiliwa kwa dhamana

Balala, watuhumiwa wengine wawili waachiliwa kwa dhamana

0
kra

Waziri wa zamani wa Utalii Najib Balala pamoja na watuhumiwa wengine wawili wameachiliwa kwa dhamana. 

Balala aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 au shilingi milioni moja pesa taslimu baada ya kutokiri mashtaka 10 ya madai ya wizi wa shilingi bilioni 8.5 za ujenzi wa Chuo cha Utalii cha Ronald Ngala.

kra

Balala alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Malindi Joseph Mwaniki akishtakiwa pamoja na aliyekuwa katibu katika wizara yake Leah Gwiyo na Joseph Odero mwenye umri wa miaka 82.

Mahakama pia iliagiza Odero kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3 na mdhamini wa kiasi kama hicho cha fedha au shilingi laki 8.

Wale wanaokabiliwa na mashtaka ni 17 lakini ni watatu tu waliokamatwa ingawa ofisi ya kiongozi wa mashtaka iliitaka mahakama kutoa vibali vya kukamatwa kwa washukiwa waliosalia.

 

Dickson Wekesa
+ posts