Home AFCON 2023 Bafana waangusha Simba wa Atlas na kufuzu robo fainali AFCON

Bafana waangusha Simba wa Atlas na kufuzu robo fainali AFCON

0

Afrika Kusini waliendeleza ubabe wao dhidi ya Atla Lions ya Morocco baada ya kuwacharaza magoli 2-1 katika mechi ya mwisho ya awamu ya 16 bora iliyopigwa Jumanne usiku mjini San Pedro.

Afrika kusini walichukua uongozi katika dakika ya 57 kupitia kwa Evidence Magkopa kabla ya Teboho Mokoena kuongeza la pili mwishoni mwa mechi.

Atlas Lions watajilaumu baada ya Hakimi Achraf kupoteza penati na baadaye Sofiane Amrabat akakishwa kadi nyekundu.

Bafana walifuzu kwa robo fainali ambapo wameratibiwa kuchuana na Cape Verde.

Website | + posts