Bafana Bafana ya Afrika Kusini na Chui wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watashuka katika uchanjaa wa Félix Houphouët-Boigny mjini Abidjan, Jumamosi usiku katika pambano la kuwania nafasi ya tatu na nne.
Ndoto ya Congo kucheza fainali ya AFCON ilizimwa na wenyeji Ivory Coast, baada ya kusakamwa bao moja bila jibu katika nusu fainali ,wakati Bafana wakishindwa na Nigeria penati 4-2 baada ya sare ya 1-1 katika semi fainali.
Timu zote zinajivunia kuwa na wachezaji wengi tajika wachezaji takriban wote wa Congo wakipiga soka ya kulipwa Ulaya, huku wachezaji wote wa Afrika Kusini wakicheza katika ligi ya nyumbani wengi wakitokea klabu ya Mamelodi Sundowns.
Mchuano huo utang’oa nanga saa tano usiku mida ya Afrika mshariki.
Congo wameshinda mechi zote mbili za awali za kuwania nafasi ya tatu katika kipute cha AFCON, huku Afrika Kusini walioshinda mechi ya nafasi ya tatu mwaka 2000 wakijivunia kutoshindwa na Congo.