Home Kaunti Baadhi ya ng’ombe walioibwa kutoka shamba la Mugie wapatikana

Baadhi ya ng’ombe walioibwa kutoka shamba la Mugie wapatikana

Baadhi ya ng’ombe ambao walioibwa kutoka kwenye shamba la Mugie lililo katika kaunti ya Laikipia wamepatikana.

Runinga ya KBC iliangazia taarifa ya wizi wa mifugo hao uliotekelezwa Januari 2,2024.

Wezi wapatao 60 waliokuwa wamejihami walivamia shamba hilo usiku huo na kutoweka na ng’ombe 256.

Msimamizi wa shamba hilo Ivan Tomlinson amethibitisha kwamba maafisa wa usalama wamefanikiwa kupata ng’ombe 99 kwenye vijiji tofauti vya kaunti ya Samburu.

Tomlinson sasa anatoa wito kwa waziri wa mambo ya ndani Profesa Kithure Kindiki kuimarisha juhudi za kukabiliana na ujangili katika eneo hilo.

Aliongeza kusema kwamba ukosefu wa usalama katika kaunti za Laikipia, Samburu, Isiolo na Baringo umelemaza maendeleo ya kitaifa ikitizamiwa kwamba mashamba makubwa hutoa mchango muhimu kupitia nafasi za ajira na ushuru.

Website | + posts
Lydia Mwangi
+ posts