Home Kimataifa Kukandamizwa kwa waandamanaji? Azimio yatishia kwenda ICC

Kukandamizwa kwa waandamanaji? Azimio yatishia kwenda ICC

0
kra

Muungano wa Azimio umetishia kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC kufuatia kile unachodai ni ukatili waliofanyiwa waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka aliyewaongoza viongozi wengine wa muungano huo katika kuwatembelea majeruhi wa maandamano hayo katika hospitali ya kitaifa ya rufaa ya Kenyatta, KNH.

kra

“Watoto wetu, Gen Z, walijitokeza kwa amani katika mitaa yetu, mamia kwa maelfu, kupinga madhila ya kijamii na kiuchumi wanayokumbana nayo Wakenya kutokana na uongozi mbaya wa Kenya Kwanza. Wameuawa, kushambuliwa kikatili na kutekwa nyara,” alidai Kalonzo.

“Kama wakili, tutanakili kila kesi na tutaiwasilisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC. Huu ni uhalifu dhidi ya binadamu.”

Matamshi yake yanakuja wakati polisi wamelaumiwa kwa kuwafyatulia risasi waandamanaji waliodumisha amani wakati wa maandamano hayo.

Chama cha Wanasheria nchini, LSK na Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu, KNHCR ni miongoni mwa mashirika yaliyokuwa mstari wa mbele kuwanyoshea polisi kidole cha lawama.

Angalau watu 20 wameripotiwa kufariki kutokana na maandamano hayo huku mamia ya wengine wakisemekana kujeruhiwa.