Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja One Kenya umeshutumu kukamatwa kwa viongozi wake juzi Jumanne.
Kinara wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amelaani vikali kutiwa mbaroni kwa viongozi kadhaa akiwemo mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino.
Imebainika kuwa Owino alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Wang’uru baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA punde baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Maandamano yaliyoitishwa na Azimio yameingia siku ya pili leo Alhamisi huku watu sita wakiripotiwa kufariki.