Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja Raila Odinga amesema wako tayari kuzungumza na serikali kuhusu maswala yanayoikumba nchi.
Akizungmza Jumanne baada ya kukutana na wabunge wa upinzani, Raila amekariri kujitolea kuhakikisha mazungumzo hayo yanazaa matunda.
Muungano wa upinzani jana Jumatatu uliteua jopo la wanachama watano watakaoshiriki mazungumzo na upande wa serikali.
Jopo hilo linawajumuisha kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa wachache katika bunge la taifa Opiyo Wandayi, Eugene Wamalwa, Seneta wa Nyamira Okong’o Omogeni na mbunge wa Malindi Amina Mnyanzi.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuongozwa na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo.
Maswala yaliyotolewa na Azimio kwa mazungumzo ni pamoja na gharama ya juu ya maisha,ukaguzi wa matokeo ya Urais mwaka uliopita ,kubuniwa kwa tume huru ya mipaka na uchaguzi,ujumuishwaji wa kila mmoja katika maswala ya kitaifa na kuheshimu sheria za vyama vya kisiasa kulingana na katiba.