Home Habari Kuu Awamu ya mwisho ya Vision 2030 yazinduliwa

Awamu ya mwisho ya Vision 2030 yazinduliwa

0

Serikali imezindua awamu ya nne na ya mwisho ya Mpango wa Maendeleo wa Vision 2030, unaojulikana kama Mpango wa Nne wa Muda wa Kati (MTP IV).

Awamu hiyo inayojumuisha kipindi cha mwaka 2023 hadi 2027 inalenga kubadilisha Kenya kuwa nchi mpya ya kiviwanda na ya kipato cha kati ifikapo 2030.

Ili kuhakikisha maendeleo yaliyoratibiwa, MTP IV inawiana na Mipango ya Maendeleo ya Kaunti (CIDPs) ya kaunti zote 47, ikijumuisha Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya Kuanzia Chini hadi Juu (BETA).

BETA inaangazia uwekezaji wa kimkakati katika kilimo, afya, makazi, biashara na uchumi wa kidijitali na ubunifu ili kuimarisha nguzo za kiuchumi, kisiasa na kijamii za Kenya Vision 2030.

Katika kipindi cha MTP IV, serikali inanuia kuimarisha programu na miradi inayoendelea kote nchini ili kuongeza thamani ya na hivyo kukuza kipato cha wananchi.

Hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika kaunti ya Marsabit iliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki na kuwashirikisha washikadau wa MTP-IV kwa kuelezea mipango na miradi ya maendeleo iliyopangwa kwa kaunti ya Marsabit hadi 2027.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Idara ya Maeneo Kame Kello Harsama, Gavana wa Marsabit Mohamed Mohamud Ali, maafisa wakuu wa serikali ya kitaifa na kaunti na wawakilishi wa jamii.

Rahab Moraa
+ posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here