Home Habari Kuu AU yataka Ethiopia na Somalia kumaliza mzozo wa bahari

AU yataka Ethiopia na Somalia kumaliza mzozo wa bahari

0

Kamati ya usuluhishi wa mizozo ya Umoja wa Afrika, AU imeyataka mataifa ya Ethiopia na Somalia kumaliza mzozo baina yao.

Mataifa ya Somalia na Ethiopia yamekuwa yakizozania bahari ya Somalia ambayo Ethiopia waliafikiana kuitumia kwa shughuli zake za kibiashara.

Hata hivyo, licha ya makubaliano, Somalia walibadali msimamo na kujiondoa kwenye mkataba, hali ambayo imezua tumbo joto kati ya nchi hizo.

AU inahofia kuwa mchecheto kati ya mataifa hayo huenda ukazua mzozo mkubwa katika upembe wa Afrika Mashariki.