Arsenal imeafikia makubaliano ya kumsajili nahodha wa Westham United Declan Rice kwa ada ya pauni 105 baada ya ofa mbili za awali kukataliwa.
Manchester City walijiondoa katika kinyangányiro cha kumsaini kiungo huyo baada ya ofa za awali kukataliwa .
Arsenal tayari imeafikia kuhusu matakwa ya kibinafsi ya mchezaji huyo.
Klabu hiyo pia imetangaza kumsaini Kai Havertz kutoka Chelsea kwa pauni milioni 67 nukta .