Home Habari Kuu Ardhi ya serikali iliyonyakuliwa Laikipia kutwaliwa

Ardhi ya serikali iliyonyakuliwa Laikipia kutwaliwa

Inaaminika kuwa ardhi nyingi iliyonyakuliwa iko katika miji ya Nanyuki na Nyahururu.

0
Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Laikipia Mashariki Patrick Muli.

Serikali imeanzisha mchakato wa kutwaa ardhi yake iliyonyakuliwa na wastawishaji wa kibinafsi katika kaunti ya Laikipia.

Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Laikipia Mashariki Patrick Muli, alisema serikali iko makini kuhakikisha ardhi yote ya serikali iliyonyakuliwa, ili kutumika kwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika kaunti hiyo.

“Ardhi nyingi ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti, iko mikononi mwa wanyakuzi ardhi. Mipango inaendelea ya kutwaa ardhi hiyo ili itumike katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,”alisema Muli.

Muli aliyasema hayo siku ya Ijumaa, alipokuwa akikabidhi ardhi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, akiongeza kuwa ardhi nyingi iliyonyakuliwa iko katika miji ya Nanyuki na Nyahururu.

Alisema katika muda wa wiki chache zijazo, serikali ya kitaifa itazindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.

Website | + posts