Home Michezo APR kungwangurana na Red Arrows fainali ya kombe la CECAFA

APR kungwangurana na Red Arrows fainali ya kombe la CECAFA

0
kra

Mabingwa wa Rwanda ,APR watachuana na mabingwa wa Zambia Red Arrows Jumapili alasiri katika fainali ya  mwaka huu ya kombe la vyama vya soka Afrika Mashariki na kati,CECAFA jijini Dares Salaam ,Tanzania.

APR walijikatia tiketi kwa fainali baada ya kuwapiku Al Hilal kutoka Sudan penati 5-4, kufuatia sare tasa katika nusu fainali ya  Ijumaa, huku Red Arrows ikiwakomoa Al Wahdi SC ya Sudan magoli mawili bila jibu katika semi fainali .

kra

Al Hilal watapimana nguvu na  Al Wahdi kuwania nishani ya shaba kabla ya kupisha fainali.

Waakilishi pekee wa Kenya,Gor Mahia walibanduliwa katika hatua ya makundi wakisajili sare moja na kupoteza mechi mbili dhidi ya Red Arrows na Al Hilal.

Mashindano hayo yanaandaliwa katika uwanja wa Azam Sports Complex na ule wa KMC.

 

Website | + posts