Home Michezo Anthony Martial athibitisha kuondoka Manchester United

Anthony Martial athibitisha kuondoka Manchester United

0

Mshambulizi wa Ufaransa Anthony Martial amethibitisha kuwa ataondoka katika klabu ya Manchester United, baada ya kuwachezea kwa miaka tisa.

Katika ujumbe alioutuma kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, nyota huyo alitaja ufanisi wake akiwa uwanjani Old Traford na kuwashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na klabu hiyo  kwa uhamisho wa pauni milioni 36 kutoka Monaco Septemba 2015, lakini alishindwa kutimiza matarajio.

Hata hivyo Martial hajaichezea klabu hiyo katika mechi yoyote tangu Desemba, baada ya kufanyiwa upasuaji wa paja.

Akiwa na Man U, Martial alishinda Kombe la FA,a Ligi kuu, Ligi ya Europa lakini hakufanikiwa kutwaa kombe la Ligi  ya Mabingwa.

Kwa jumla alicheza mechi 317 na  kufunga mabao 90 na kuchangia mengine 47.

Mkataba wa Martial  na Man United ulikuwa ukamilike  mwezi Julai.