Home Habari Kuu Angola yajiondoa katika shirika la wazalishaji mafuta la OPEC

Angola yajiondoa katika shirika la wazalishaji mafuta la OPEC

0
kra

Angola imetangaza kujiondoa katika shirika la wazalishaji wa mafuta la Opec kutokana na mzozo wa mgawo wa pato.

Inafuatia uamuzi wa mwezi uliopita wa shirika hilo lenye wanachama 13 na mataifa 10 washirika kupunguza zaidi uzalishaji wa mafuta mnamo 2024 ili kuongeza bei ya kimataifa.

kra

Kwa sasa Angola inazalisha takriban mapipa milioni 1.1 kwa siku, kati ya milioni 30 kutoka Opec nzima.

Bei ya mafuta ilishuka kwenye habari, huku bei ya Brent ikipungua zaidi ya $1 hadi $78.5 kwa pipa ifikapo 12:50 GMT, Reuters inaripoti.

Uamuzi wa Angola wa kujiondoa kwenye OPEC ulikuja katika mkutano waAlhamisi wa baraza la mawaziri.

“Tunahisi kwamba kwa wakati huu Angola hainufaiki chochote kwa kubaki katika shirika na, katika kulinda maslahi yake, iliamua kuondoka,” Waziri wa Rasilimali Madini na Petroli Diamantino Azevedo alisema baadaye.

“Kama tungebakia OPEC… Angola ingelazimika kupunguza uzalishaji, na hii inakwenda kinyume na sera yetu ya kuepuka kushuka na kuheshimu mikataba.”

Waziri huyo aliongeza kuwa uamuzi huo haukuchukuliwa kirahisi.

Angola na Nigeria ni wauzaji wakubwa wa mafuta katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa.

Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa nchi hizo mbili hazijafurahishwa na mpango wa kupunguza uzalishaji wakati zinahitaji kuongeza mapato yao ya fedha za kigeni.

Angola ina hifadhi kubwa ya madini na petroli, na uchumi wake ni miongoni mwa unaokuwa kwa kasi zaidi duniani – lakini ukuaji wa uchumi hauko sawa.

Sehemu kubwa ya utajiri wake wa mafuta upo katika jimbo lake tofauti la Cabinda, ambapo mzozo wa miongo kadhaa wa kujitenga unazuka.

Angola – ambayo ilikuwa mwanachama wa Opec kwa miaka 16 – sio nchi ya kwanza kuondoka kwenye shirika hilo. Ecuador, Indonesia na Qatar zote zimefanya sawa.

Opec ni kundi la wazalishaji wa mafuta ambalo huamua ni kiasi gani cha mafuta ghafi ya kuuza kwenye soko la dunia, pamoja na kundi lililopanuliwa liitwalo Opec+.

BBC
+ posts