Angalau maafisa 4,000 kutoa usalama wakati wa Mkutano wa Tabia Nchi Nairobi

Martin Mwanje
1 Min Read

Maafisa wa usalama wasiopungua 4,000 watakaa chonjo kuhakikisha usalama wa wote watakaohudhuria Mkutano wa Tabia Nchi wa Afrika. 

Mkutano huo utafanyika katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la Kenyatta, KICC kuanzia Septemba 4-8, 2023.

Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo amesema serikali pia imeandaa mpango madhubuti wa kuitikia hali za dharura zisizotazamiwa haraka iwezekanavyo.

Dkt. Omollo aliyasema hayo leo Jumanne wakati wa mkutano wa pili wa kuangazia hali ya usalama wakati wa Mkutano wa Tabia Nchi wa Afrika.

Mkutano wa leo Jumanne ulihudhuriwa na jumuiya ya kidiplomasia na mashirika ya kimataifa.

Wajumbe na viongozi wasiopungua 14,000 wanatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Tabia Nchi wa Afrika, miongoni mwao Wakuu kadhaa wa Nchi na Mawaziri kutoka kanda hii na kote duniani.

Website |  + posts
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *