Home Michezo Andiego anusia kuwahi tiketi ya Olimpiki Paris

Andiego anusia kuwahi tiketi ya Olimpiki Paris

Bondia Elizabeth Adiego wa Kenya alikaribia kuwahi tiketi ya michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao jijini Paris Ufaransa baada ya kutinga nusu fainali ya mashindano ya Afrika jijini Dakar Senegal , alipomzaba Ornella Sathoud kutoka Ghana pointi 5 kwa bila katika robo fainali ya uzani wa kadri .

0

Andiengo ambaye ni naibu nahodha wa timu ya Kenya maarufu kama Hitsquad atazichapa dhidi ya chipukizi wa Tunisia Molka Mabrouk aliye na umri wa miaka 19, katika hatua ya nusu fainali huku mshindi akifuzu kwenda Paris mwakani.

Katika pigano jingine Teresiah Wanjiru alizidiwa na mshindi wa nishani ya shaba ya shaba ya michezo ya jumuiya ya madola Cynthia Ogunsemilore kutoka Nigeria na kumlazimu mwamuzi kusitisha pigano ili kumwokoa Mkenya.

Website | + posts