Home Kimataifa ANC na DA vyakubaliana kubuni serikali ya umoja wa kitaifa

ANC na DA vyakubaliana kubuni serikali ya umoja wa kitaifa

0
kra

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini, Democratic Alliance (DA), kimesema kimekubaliana na chama tawala cha African National Congress (ANC) kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Haya yanajiri baada ya wiki kadhaa za uvumi kuhusu nani ANC itashirikiana naye baada ya kupoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

kra

ANC ilipata 40% ya kura, huku DA ikishika nafasi ya pili kwa 22%.

Hii inafungua njia kwa kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa kubakia ofisini kama rais.

Muungano kati ya chama cha mrengo wa kati DA na ANC haujawahi kutokea kwani vyama hivyo viwili vimekuwa hasimu kwa miongo kadhaa.

Chama cha ANC kikiongozwa na Nelson Mandela kilimaliza mfumo wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994 na kushinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo.

Wakosoaji wa DA wameishutumu kwa kujaribu kulinda haki za kiuchumi ambazo wazungu wachache nchini humo walijenga wakati wa ubaguzi wa rangi, madai ambayo chama hicho kinakanusha.

Kiongozi wa DA John Steenhuisen alisema mpango huo ni “Mwanzo mpya katika historia yetu”.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa kurejeshauungwaji mkono wa DA kwa Bw Ramaphosa, ANC itamuunga mkono Annelie Lotriet wa DA kama naibu spika wa bunge.

Pia alisema utaratibu wa kugawana madaraka utahusisha nyadhifa za baraza la mawaziri kwa DA ambacho hadi sasa kimekuwa chama cha upinzani.

Mkataba huo pia unajumuisha Inkatha Freedom Party (IFP), chama cha kihafidhina chenye ufuasimkubwa wa Wazulu, ambacho kilipata asilimia 4 ya kura, na Muungano wa Patriotic Alliance (PA), ambao unapata kuungwa mkono na jamii ya watu wa rangimbali mbali – kama wanavyojulikananchini Afrika Kusini.

Tovuti ya habari ya Afrika Kusini News24 inasema makubaliano hayo pia yanahusu serikali za majimbo ya Gauteng na KwaZulu-Natal.

Steenhuisen alisema: “Kupitia kura, nchi imeweka wazi kuwa haitaki chama kimoja kutawala jamii yetu.”

Inatajwa kuwa ni Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU), lakini ANC ilishindwa kupata vyama vya tatu na vya nne kwa ukubwa – chama cha UMkhonto weSizwe (MK) cha Rais wa zamani Jacob Zuma na Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema – kujiunga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here