Home Kimataifa Amos Wako: Ipo haja ya kuzifanyia marekebisho sheria za uchaguzi

Amos Wako: Ipo haja ya kuzifanyia marekebisho sheria za uchaguzi

Wako anapendekeza kuandaliwa kwa mashauriano kuhusu janga la kiuchumi, ili kujadili mbinu za kupunguza gharama ya maisha.

0
kra

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Amos Wako amesema wakati umewadia kwa bunge la kitaifa kufanyia marekebisho sheria za uchaguzi ili kuwezesha seva kuwa wazi kwa Wakenya wote baada ya uchaguzi mkuu. 

Alipofika mbele ya kamati ya kitaifa ya majadiliano, Seneta huyo wa zamani wa Busia, alitaka upande wa upinzani kuhusishwa katika mchakato wa kubuni tume ya uchaguzi nchini ili kuimarisha uwazi katika uchaguzi.

kra

Kulingana na Wako, ipo haja kwa mfumo wa uchaguzi hapa nchini kuiga mbinu bora za uchaguzi kutoka zile za kihistoria ili kuzuia kesi za kiuchaguzi.

Wako alipendekeza kuwa vyama vikuu vitatu nchini viwe na uwakilishi katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC.

Wakati  huohuo, Wako anapendekeza kuandaliwa kwa mashauriano kuhusu janga la kiuchumi ili kujadili mbinu za kupunguza gharama ya maisha.