Home Kimataifa Amayo, Esipisu watemwa katika uteuzi wa hivi punde wa mabalozi

Amayo, Esipisu watemwa katika uteuzi wa hivi punde wa mabalozi

0

Rais William Ruto amefanya uteuzi watu 43 watakaohudumu kama mabalozi na manaibu mabalozi katika nchi za kigeni na katika nyadhifa zingine mbalimbali.

Baadhi ya wanasiasa wanaounga mkono serikali ya Kenya Kwanza na baadhi waliokuwa wameteuliwa kuhudumu kama manaibu wa mawaziri (CAS) wamenufaika na uteuzi huo.

Miongoni mwao ni aliyekuwa mbunge wa Nyando ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Misri.

Naibu Gavana wa zamani wa kaunti ya Kisii Joash Maangi kwa upande mwingine ameteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Uganda.

Aliyekuwa Seneta mteule Petronila Were ameteuliwa kuhudumu kama naibu balozi wa Kenya nchini Ethiopia.

Katika uteuzi huo, nafasi ya Manoah Esipisu itachukuliwa na Catherine Kirumba Karemu aliyeteuliwa kuhudumu kama balozi wa Kenya nchini Uingereza.

Kwa upande mwingine, nafasi ya Balozi Lazarus Amayo nchini Marekani itachukuliwa na David Kiplagat Kerich.

Wengine walioteuliwa kuhudumu kama mabalozi ni Lilian Tomitom (Zambia), Vincent Mogaka Kemosi (Ghana, Profesa Anne Kisaka Nanguli (Senegal), Luteni Jenerali Peter Mbogo Njiru (Pakistan), Timothy Kaluma Mcharo (Algeria) na Caroline Kamende Daudi (Canada).

Jessica Muthoni Gakinya ameteuliwa kuhudumu kama Balozi wa Kenya nchini Morocco, Halima Yussuf Mucheke (Uholanzi), Everylyne Mwenda Karisa (Cuba), Dkt. Peter Mutuku Mathuki (Urusi), Moi Lemoshira (Japan), Kenneth Milimo Nganga (UAE), Luteni Jenerali Jonah Mwangi (Iran) na Abdi Aden Korio (Oman).

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, CA Ezra Chiloba ameteuliwa kuhudumu kama mkuu wa ubalozi mdogo wa Kenya mjini Los Angeles nchini Marekani miongoni mwa wengine walioteuliwa kuhudumu katika nyadhifa mbalimbali.

Majina ya walioteuliwa yamepelekwa bunge ili kupigiwa msasa kabla ya Rais kuwateua rasmi kuhudumu katika nyadhifa hizo.

 

 

Website | + posts