Aliyekuwa katibu wa teknolojia ya habari Sammy Itemere, pamoja na washtakiwa wenza, wameachiliwa huru katika kesi iliyowakabili ya wizi wa shilingi milioni 122.
Washukiwa hao waliachiliwa huru baada ya hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Lucas Onyina kuwaondolea mashtaka, akiwemo naibu gavana wa Kakamega Ayub Savula.
Hatua hiyo ilitokana na ombi lililowasilishwa na kiongozi wa mashtaka ya umma Renson Mulele, la kumtaka hakimu huyo kufanya hivyo kutokana na ukosefu wa Ushahidi wa kutosha dhidi ya wasukiwa hao.
Ombi hilo liliungwa mkono na hakimu huyo baada ya kupitia ushahidi uliotolewa. Mahakama vile vile imeagiza 13 hao warudishiwe dhamana ya pesa taslimu walizotoa.
Baada ya hatua hii, upande wa mashtaka umetuma ombi la kuwaondlea 13 hao kati ya washukiwa 22 na pia kupewa muda wa kuandaa Ushahidi halisi dhidi ya washtakiwa tisa waliosalia katika kesi hiyo.
Savula and his co-accused allegedly stole Ksh 122 million in Government advertising.