Home Kimataifa Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Burundi akamatwa

Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Burundi akamatwa

Murengerantwari alikuwa ameteuliwa kuongoza benki kuu ya Burundi kwa miaka mitano kuanzia mwezi Agosti mwaka jana.

0

Gavana wa benki kuu ya Burundi aliyefutwa kazi hivi majuzi amekamatwa kwa tuhuma za ufisadi.

Dieudonné Murengerantwari ameshutumiwa na wizara ya sheria kwa “kuhujumu utendakazi mzuri wa uchumi wa taifa, ufisadi wa kimya kimya, ufujaji wa pesa na ufujaji wa mali ya umma”.

Hajajibu tuhuma zinazomkabili.

Siku ya Jumapili, Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye alimfukuza kazi Bw Murengerantwari na nafasi yake kuchukuliwa na Édouard Normand Bigendako.

Murengerantwari alikuwa ameteuliwa kuongoza benki kuu ya Burundi kwa miaka mitano kuanzia mwezi Agosti mwaka jana.

Mwanasheria Mkuu Leonard Manirakiza Jumanne alisema kuwa madai dhidi ya Bw Murengerantwari ni ya muda huku uchunguzi ukiendelea.

Pia alisemautaratibu wa sheria unafuatwa huku Bw Murengerantwari akiendelea kuzuiliwa.